Jumamosi 9 Agosti 2025 - 14:08
Hoja za wilayat Faqihi (Hoja ya Kinakili)

Hawza /Wafuasi wa Imam wa zama (as) katika kipindi cha ghaiba ya huyo mtukufu wanapaswa katika masuala yanayojitokeza kumrejea mpokezi wa hadithi, ni wazi kuwa kuelewa maneno ya Ma‘sumiin (as) kuhusu hukumu na majukumu ya mtu binafsi au kijamii kunahitaji utaalamu wa hali ya juu mno katika elimu za Kiislamu na kidini, na kupata hukumu za kisheria kutoka na hadithi za Maimamu ni jambo lenye ugumu mkubwa.

Shirika la Habari la Hawza - Miongoni mwa hoja muhimu zaidi za wilayat faqihi ni riwaya, na baadhi yake tunazinukuu hapa:

Tawqi‘(1) ya Imam wa zama (as)
Mwanachuoni mkubwa wa Kishia, Sheikh Ṣadūq (r.a) katika kitabu chake "Kamal al-Din wa Tamam al-Ni‘ma", amepokea barua ya Isḥāq bin Ya‘qub kwa Imam Mahdi (as), Ndani ya barua hiyo maswali fulani yaliulizwa mbele ya Imam.

Imam wa zama (as) katika jibu lake amesema:

«وَ أَمَّا الْحَوَادِثُ الْوَاقِعَةُ فَارْجِعُوا فِیهَا إِلَی رُوَاةِ حَدِیثِنَا فَإِنَّهُمْ حُجَّتِی عَلَیْکُمْ وَ أَنَا حُجَّةُ اللَّهِ عَلَیْهِمْ.» 

"Na ama kuhusu masuala yanayojitokeza, basi katika hayo warejeeni wapokezi wa hadithi zetu; kwani wao ni hoja yangu juu yenu na mimi ni hoja ya Mwenyezi Mungu juu yao."

(Kamal al-Din wa Tamam al-Ni‘ma, Juz. 2, uk. 484)

Katika sehemu ya kwanza ya tawqi‘, Imam (as) ameamuru kwamba Mashia katika zama za ghaiba warejee kwa wapokezi wa hadithi za Ahlul-Bayt (as) na wawaulize kuhusiana na wajibu wao katika masuala ya dharura na yanayojitokeza.

Ni lazima kutafakari kuwa ni nani wanaokusudiwa na neno "rūwāt ḥadīthinā" (رواة حديثنا) na maana ya "ḥawādith wāqi‘a" (حوادث واقعة) ni ipi?
Neno "ḥawādith" ni wingi wa "ḥāditha" (tukio), na kwa kuwa Imam amesema: katika matukio yanayotokea warejeeni wapokezi wa hadithi, inadhihirika kwamba makusudio ya matukio hayo ni masuala yanayohusiana na dini na diwani ya Waislamu ambayo wapokezi wa hadithi wanapaswa kubainisha wajibu wa waumini ndani yake.

Sasa swali ni hili: je, makusudio ni masuala ya mtu binafsi kama yalivyoelezwa katika risala za kielimu, au ni masuala ya kijamii kama vile jihadi dhidi ya makafiri, kujihami mbele ya uvamizi wa wageni, mahusiano ya kisiasa, kiuchumi na kitamaduni na serikali za kigeni, na mengineyo?
Ni jambo lisilo la kawaida kudhani kwamba makusudio ya Imam wa zama (as) kuhusu "ḥawādith wāqi‘a" ni masuala binafsi kama vile swala, saumu, zakat na mengineyo; kwani kurejea kwa wanazuoni wa dini na kuwauliza kuhusu masuala haya hata katika zama za Maimamu (as) kulikuwa ni jambo la kawaida, na Mashia kutokana na sababu kama umbali wa safari au vizuizi vilivyokuwa vikimkabili Imam (as), walikuwa wakiwarejea mawakala na manaibu wa Maimamu (as).

Kwa hakika jambo hili lilikuwa ni la wazi kwamba pale ambapo haiwezekani kumfikia Imam Maasumu (as) iwe katika wakati ambapo Imam yupo dhahiri na anaonekana au wakati yupo katika ghaiba, ni lazima kumrejea mwanachuoni wa dini anayefahamu Qur’an na Sunna.
Kwa hiyo, makusudio ya "ḥawādith wāqi‘a" ni masuala ya kijamii ya Waislamu, na maana hii inalingana kikamilifu na dhahiri ya tamko "hawādith".

Wapokezi wa hadithi za Maimamu ni kina nani?
Kwa mujibu wa tawqi‘ ya Imam wa zama (as), wafuasi wa huyo mtukufu katika zama za ghaiba wanapaswa katika masuala yanayojitokeza kumrejea mpokezi wa hadithi, ni wazi kuwa kuelewa maneno ya Ma‘sumiin (as) kuhusiana na hukumu na majukumu ya mtu binafsi na ya kijamii kunahitaji utaalamu wa juu mno katika elimu za Kiislamu na kidini, na kupata hukumu za kisheria kutoka katika hadithi za Maimamu ni jambo gumu sana.l, ndio maana tangu zamani, Mashia walikuwa wakiwarejea wanachuoni na wajuzi wa kweli wa Uislamu kwenye jambo hili.

Hivyo basi, makusudio ya mpokezi wa hadithi si yule anayenukuu hadithi pekee; bali ni yule ambaye kwanza anao ufahamu kamili wa vyanzo vya riwaya na anatambua riwaya sahihi na ile isiyo sahihi, na pili anayefahamu pande zote za maneno ya Ma‘sumiin na namna ya kupata hukumu ya kisheria kutokana na maneno yao, na amejipatia maandalizi na nyenzo zote muhimu kwa ajili ya uelewa sahihi wa maneno yao.

Kwa kukiri kwa Waislamu wote na watu wote wa akili na fikra, watu wa aina hii si wengine bali ni mafaqihi na majitahida wa kidini wanaotoa hukumu za Mwenyezi Mungu katika masuala yote ya mtu binafsi na kijamii kutoka katika Qur’an na maneno ya Ma‘sumiin, na kuziweka hukumu za masuala yote mikononi mwa Mashia.

Maelezo haya yanalingana na sehemu ya mwisho ya hadithi ambapo amesema:

 «فَإِنَّهُمْ حُجَّتِی عَلَیْکُمْ»

kwa sababu hiyo kuwa mpokezi inalingana na mambo ambayo rai na maoni yake katika mambo hayo yanakuwa ndiyo kipimo na kigezo; yaani, wakati ambapo huyu “mpokezi wa hadithi” anakuwa hoja juu ya wengine ni pale ambapo istinbati (uchanganuzi wa kielimu) wake kutoka katika maneno ya Maasumuin unakuwa hoja kwa wengine, na lau kama ingelikuwa ni kurejea moja kwa moja kwenye maneno ya Maasumuin, asingesema: wao wenyewe ni hoja juu yenu.

Kuhusu jambo hili, kauli ya faqihi mkubwa na mashuhuri wa Kishia, Sheikh Ansari (r.a), ni yenye maelezo ya wazi kabisa, ambapo amesema:
Kinachofahamika kutokana na dhahiri ya kauli ya Imam ni kwamba makusudio ya "ḥawādith" ni mambo yote ambayo kwa mujibu wa desturi ya kijamii (‘urf), akili, na sharia, katika hayo inapaswa kurejea kwa kiongozi na [mkuu wa jamii], na ni jambo lisilo la kawaida kudhani kuwa "ḥawādith" imehusu tu masuala ya kisheria.

(Makāsib al-Muḥarrama, Juz. 3, uk. 554)

Utafiti huu unaendelea...

Imenukuliwa kutoka katika kitabu kiitwacho "Negin Āfarinish", huku ikifanyiwa mabadiliko madogo.

1. Tawqi‘ ni istilahi inayotumika zaidi kuhusu barua za Imam wa zama as. Ndani ya barua hizo, majibu ya maswali ya Mashia yaliandikwa na kufikishwa kwao kupitia "nawwab arba‘a" (manaibu wanne).

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha